
Mwanachama wa ACT Wazalendo, Luhaga Mpina amekataa kukutana na Tume ya Rais ya Kuchunguza Matukio ya Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, akidai kuwa chama chake kilishaweka wazi kuwa hakitatoa ushirikiano wowote kwa sababu hakina imani na tume hiyo.
Mpina amesema tume hiyo ni chombo kisicho huru na kimeundwa bila kuzingatiwa kanuni na taratibu za usuluhishi wa migogoro.
Mpina amesema “Chama cha ACT Wazalendo kiliweka wazi kwamba hakitashiriki kwa namna yoyote ile katika uchunguzi utakaofanywa na tume hii. Hatutatoa ushahidi wala kutoa ushirikiano wowote kwani tunatambua kuwa ni chombo kisicho huru na kitakachotegemea maagizo ya serikali.”







