
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imekubali pingamizi lililowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari dhidi ya uteuzi wa Mgombea Urais wa Tanzania kupitia ACT-Wazalendo, Luhaga Mpina.
Kufuatia pingamizi hilo, INEC imeondoa jina la Mpina kwenye orodha ya wagombea wa Urais wa Tanzania mwaka 2025.
Aidha, INEC imetupilia mbali pingamizi la Mgombea Urais kupitia NRA, Almas Kisabya na Mgombea Urais kupitia chama cha AAFP, Kunje Mwiru dhidi ya uteuzi wa Luhaga Mpina kukosa sifa za kugombea nafasi hiyo.
Hata hivyo, INEC imetupilia mbali pingamizi lililowekwa na Mpina dhidi ya uteuzi wa Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi, Rais Samia Suluhu.








