Lushoto: Wazee wakausha maji baada ya mradi kuanzishwa bila kupewa taarifa

0
70

Wakazi wa Kata ya Kwekanga wilayani Lushoto mkoani Tanga wamekumbana na ukosefu wa maji baada ya wazee wa kata hiyo kudaiwa kuzuia chanzo cha maji kutotoa maji hadi kufanyike tambiko, baada ya mkandarasi kuanza mradi bila kuwashirikisha.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara, Meneja wa Mamlaka ya Maji (RUWASA) Wilaya ya Lushoto, Mhandisi Erwin Sizinga amesema walifanya kikao na wananchi wakawaeleza kuwa kuna chanzo cha maji kinachopatikana kwenye kata hiyo, lakini walipofanya utafiti wakagundua chanzo hicho hakina maji.

“Tulipata chanzo katika kata ya jirani Kijiji cha Makole, lakini siku tunamleta mkandarasi yale maji hatukuyaona, na tulivyokaa na Serikali ya kijiji na wazee wanasema kuna matambiko kuna vitu ambavyo wamekosea kule kwenye chanzo kwahiyo tunataka kutambika, wakaomba mbuzi, njiwa tukawapa pamoja na laki na nusu lakini hadi leo maji hakuna,” ameeleza.

Naye, Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema hakuna tambiko kubwa la vyanzo vya maji kwa wakazi wa eneo hilo zaidi ya kuacha kulima kando kando ya vyanzo vya maji.

Send this to a friend