M-Bet kuzindua Stimulated Reality League (SRL)

0
75

. M-bet kuongoza ubunifu Tanzania na kuzindua SRL

· Uhalisia wa michezo kutoka M-Bet unakujia kupitia SRL

· Mechi za soka zinaendelea! Mashabiki wanaweza kumaliza msimu wa ligi kubwa za barani duniani.

M-Bet imezindua michezo ya kubashiri inayojulikana kama Simulated Reality League (SRL) , Kupitia kampuni ya SportRadar inayotoa huduma za teknolojia ya odds mbalimbali za michezo ya kubashiri, ikiwa inafanya kazi na makampuni zaidi ya 500 duniani kote.

M-bet imezindua SRL ikiwa ni ingizo jipya katika orodha ndefu ya michezo inayoendeshwa na M-bet. Ligi ya SRL ni aina mpya ya michezo inayojumuisha ubashiri wa kabla ya mechi na wakati mechi inaendelea kwa kutumia teknolojia mpya ya ubashiri kwa kutumia teknolojia ya AI(Artifcial Intelligence), SRL inatoa fursa ya kubashiri inayofanana na ile ya michezo halisi.

Michezo hii kwa sasa inahusisha ligi kubwa kutoka nchini Uingereza, Ujerumani, Italia, Uhispania na ligi nyingine za bara la Ulaya. Kila mechi ni dakika 90 na unaweza kubashiri kwa timu uipendayo, kuangalia takwimu za mechi, msimamo wa ligi pamoja na kufuatilia ubashiri wako kupitia Live in play tracker (mubashara). Uwepo wa SRL unawapa fursa mashabiki wa ligi za soka za barani Ulaya kuweza kumalizia msimu kama ilivyokusudiwa huku mechi zote zikichezwa kama ratiba ya ligi ilivyopangwa.

Uzinduzi wa michezo ya SRL unawapa fursa wateja kuweza kuendelea kufurahia michezo ya kubahatisha kwa namna ya tofauti huku wakitumia kiasi kidogo sana cha data. Ligi hii mpya inapatikana katika application za Android pamoja na kupitia tovuti www.m-bet.com/tz

Daniel Fischer, Mkurugenzi Mtendaji wa M-Bet Group amesema: Uwepo wa SRL na michezo mengine ya aina hii, inatupa fursa M-bet kuendelea kutoa huduma kwa wateja wetu walioko katika mataifa mbalimbali. Wateja wanaweza kushiriki kubashiri kabla ya mechi au wakati mechi zinaendelea katika ligi zao pendwa.Teknolojia ya Sportradar inatupa mwanga na namna ya kuweza kuendelea kuwapa burudani wateja wetu.

Send this to a friend