Maagizo 8 ya Rais Samia akizungumza na mabalozi Zanzibar

0
27

Rais Samia Suluhu Hassan leo Novemba 19, 2022 amekutana na kufanya kikao na mabalozi mbalimbali wanaoiwakilisha Tanzania katika sehemu mbalimbali duniani, ambapo katika kikao hicho ameyataja mambo muhimu ya kujadili katika mkutano huo ambao umefanyika Kisiwani Zanzibar.

Kati ya mambo ambayo Rais Samia Suluhu ameyataja kujadiliwa katika kikao hicho ni pamoja na;

1. Matishio mapya ya usalama na ustawi wa nchi yakiwemo mabadiliko ya tabia ya nchi, majanga ya afya, uhalifu wa kimataifa na mapinduzi ya nne ya viwanda.

2.Mabadiliko ya siasa za dunia ‘Global Power Politics.’

Tanzania yatoa maelekezo kwa Mabalozi wanaoiwakilisha nchi

3. Kubadilika kwa mwelekeo wa uchumi wa dunia ambapo ukuaji mkubwa wa uchumi ikiwemo uzalishaji, uwekezaji, biashara, ubunifu na uvumbuzi vimehamia kwenye bara moja la Asia.

4. Kuongezeka kwa kasi kwa utangamano katika bara la Afrika ikiwamo kupanuka kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuongezeka kwa wanachama kutoka watano hadi saba baada ya kujiunga kwa Sudan Kusini na DRC.

5. Kuanza kutekelezwa kwa itifaki ya soko huru la Afrika (African Continental Tree).

6. Kutanuka kwa matumizi ya lugha ya Kiswahili duniani pamoja na Watanzania wanaoishi nje ‘Diaspora’ jinsi wanavyochangia Tanzania na maslahi yao kule walipo.

7. Kuongeza uwajibikaji. Kuhakikisha diplomasia inakwenda na wakati, kwa ubora na ufanisi.

8. Kuajiri/kunoa waliopo na kuimarisha Wizara kwa kuhakikisha kada zote muhimu zenye kuipa uhai diplomasia zina uwakilishi kwenye Wizara.

Send this to a friend