Maagizo ya Waziri Mkuu kwa Wizara ya Nishati

0
42

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Nishati kuendelea kupanua wigo wa matumizi ya nishati ya gesi asilia ili kupunguza athari za kimazingira zinazotokana na ukataji wa misitu nchini.

Amesema hayo leo wakati alipotembelea maonesho ya majukumu ya Wizara ya Nishati na taasisi zake katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma na kusema kuwa, wizara kwa sasa iendelee kupanua wigo wa kufikia watanzania wengi zaidi katika mikoa mbalimbali nchini.

“Tupanue wigo na huduma hii iwafikie watu. Tumeanza na Dar es Salaam, tuje kwenye majiji, manispaa zetu na hata hapa Dodoma tuwe na tawi na kazi hii iendelee,” amesema.

Aidha, amewataka watendaji wote katika sekta ya nishati kuhakikisha wanasimamia upatikanaji wa nishati ya umeme na nishati nyingine ikiwemo mafuta ili kuendelea kuiwezesha nchi kupata fursa ya kuendelea kukua kiuchumi.

Send this to a friend