Maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI Tanzania yanapungua

0
56

Utafiti wa awali wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI umeonesha Tanzania imepata matokeo chanya katika mapambano dhidi ya Virusi vya UKIMWI (VVU) na UKIMWI na idadi ya maambukizi mapya inaendelea kupungua ikilinganishwa na matokeo ya utafiti kwa mwaka 2016/2017.

Akizungumza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista Mhagama amesema matokeo ya utafiti huo uliofanywa na Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) hufanyika katika ngazi ya jamii na kwa mara ya kwanza ndani ya Tanzania ulifanywa 2016/2017 ambapo kama taifa hupata nafasi ya kupima viwango vya maambukizi mapya na kupima maendeleo ya taifa katika zoezi la kufubaza Virusi vya UKIMWI katika ngazi ya kaya.

Benki Kuu: Pato la Taifa limekua kwa kiwango cha kuridhisha

“Juhudi za mapambano dhidi ya maambukizi ya UKIMWI zimeendelea kuongozwa na Rais Samia Suluhu na hii imetusaidia kuyafikia malengo ya kitaifa ya kufikia sifuri tatu yaani sifuri katika kutokuwa na maambukizi mapya, sifuri katika kuondoa unyanyapaa na ubaguzi na sifuri kwa kutokuwa na vifo vinavyotokana na UKIMWI,” amesema.

Aidha, Waziri Mhagama amesema hatua iliyofikiwa kwa sasa ni kukamilisha kuweka data na taarifa katika utaratibu unaotakiwa kisha kuzinduliwa rasmi Desemba 1, mwaka huu ikiwa na taarifa zilizojitosheleza.

Send this to a friend