Maambukizi ya UVIKO-19 nchini yaongezeka kwa 62%

0
33

Serikali kupitia Wizara ya Afya imesema katika kipindi cha Oktoba 29 hadi Desemba 02, 2022 jumla ya visa vipya 442 vimethibitika kuwa na maambukizi ya UVIKO-19

Wizara ya Afya imebainisha kuwa idadi hiyo ni kubwa ikilinganishwa na takwimu za mwezi uliopita ambapo kulikuwa na visa  vipya 272, sawa na ingezeko la asilimia 62.5.

Aidha, kwa mujibu wa ripoti hiyo katika kipindi hicho, hakuna mgonjwa aliyelazwa wala kuripotiwa kupoteza maisha kutokana na maambukizi ya UVIKO-19.

Wizara imewahimiza wananchi kujitokeza kupata chanjo ya UVIKO-19 ili kupata kinga pamoja na kuwasihi wale wote wenye dalili za ugonjwa huo kufika hospitali mara moja kwa ajili ya kupewa huduma.

Send this to a friend