Maambukizi ya UVIKO-19 yaongezeka nchini

0
42

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema maambukizi ya UVIKO-19 yanaongezeka nchini hivyo ni vyema Watanzania wakajitokeza kupewa chanjo ili kupunguza makali ya ugonjwa huo.

Amebainisha kwamba kwa wiki moja iliyopita, jumla ya watu 2,708 walipima na 160 kati yao walikutwa na maambukizi.

Ameyasema hayo jana alipokuwa akipokea msaada wa vifaa tiba vya kupima virusi vya UVIKO-19 na vifaa vya kupima kiwango cha Oksijeni mwilini uliotolewa na Serikali ya Austria kupitia kwa balozi wake nchini, Christian Fellner.

Wanaotoa fedha kwa ombaomba kushtakiwa

Amesema wamepokea jumla ya vipimo vya haraka vya UVIKO-19 katoni 2,000 vitakavyotumika kupima watu 20,000 na vipima Oksijeni 1,000 vitakavyosambazwa kwenye zahanati 500 nchini.

Aidha, ameishukuru Serikali ya Austria na kusema msaada huo utasaidia juhudi za Serikali kupambana na maambukizi ya UVIKO-19.

Send this to a friend