Mabadiliko Baraza la Mawaziri, Rais atengua uteuzi wa January Makamba, amteua Hussein Bashe

0
38

Dkt. John Pombe Magufuli amemteua George Boniface Simbachawene kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.

Simbachawene anachukua nafasi ya Mhe. January Yusuf Makamba ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Hussein Mohamed Bashe kuwa Naibu Waziri wa Kilimo.

Bashe anachukua nafasi ya Mhe. Innocent Lugha Bashungwa ambaye aliteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.

Katika hatua nyingine, Mhe. Rais Magufuli amemteua Balozi Dkt. Martin Lumbanga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA).

Balozi Dkt. Lumbanga ameteuliwa kushika nafasi hiyo kwa kipindi cha pili.

Uteuzi wa viongozi hao unaanza leo tarehe 21 Julai, 2019.

Send this to a friend