Mabaki ya panya yapatikana kwenye mikate Japan, kiwanda chasimamishwa

0
33

Kampuni maarufu ya mikate nchini Japan iitwayo Pasco Shikishima imeagiza kurejeshwa kwa maelfu ya mikate na wateja kurejeshewa pesa zao baada ya mabaki ya panya kupatikana kwenye bidhaa hiyo.

Ripoti za vyombo vya habari vya Japan vimesema watu wawili walionunua mkate huo katika Mkoa wa Gunma wamelalamikia kampuni hiyo maarufu baada ya kukumbana na mabaki ya Panya, hata hivyo hakukuwa na ripoti za mtu yeyote kupata madhara ya kiafya.

Kampuni hiyo imeomba msamaha kwa wateja walioathirika kupitia tovuti yake na kuahidi kurejesha pesa zao mtandaoni huku kiwanda kilichotengeneza mkate huo shughuli zake zikisitishwa.

Mkate wa Pasco ni chakula kikuu katika kaya nyingi za Kijapani na unapatikana kila mahali katika maduka makubwa na maduka madogo kote nchini humo, pia husafirishwa kwenda Marekani, China Australia na Singapore.

Send this to a friend