Mabalozi waeleza dhamira ya kuimarisha ushirikiano na Tanzania

0
74

Mabalozi wanaowakilisha nchi mbalimbali na taasisi za kimataifa nchini Tanzania wamethibitisha kwa pamoja dhamira yao ya kuendeleza na kuimarisha ushirikiano na Serikali ya Tanzania, hususan katika masuala ya kiuchumi.

Hayo yamebainika leo Ijumaa, Novemba 28, 2025, katika mkutano kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, na Jumuiya ya Wanadiplomasia wanaohudumu nchini.

Wanadiplomasia hao wameeleza kuwa wanaichukulia Tanzania kama mshirika muhimu na wa kuaminika katika masuala ya kikanda na kimataifa. Kadhalika, wamepongeza jitihada za Serikali katika kurejesha umoja wa kitaifa kufuatia matukio ya Oktoba 29, pamoja na hatua zinazoendelea kuchukuliwa kuimarisha amani, utawala bora na ustahimilivu wa taifa.

Akizungumza kwenye kikao hicho, Balozi Kombo amewahakikishia kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana nao kwa manufaa ya pande zote, akishirikisha pia taarifa kuhusu mwenendo wa uchaguzi mkuu, matukio yaliyofuata, na hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kulinda usalama wa wananchi, kurejesha utulivu, na kuhakikisha huduma za kijamii na shughuli za kiuchumi zinaendelea bila kusitishwa.

Send this to a friend