Mabara 5 yaliyoongoza zaidi kutembelea Zanzibar mwezi Agosti

0
44

Zanzibar ni mojawapo ya vivutio vikuu vya utalii barani Afrika na duniani. Imebarikiwa na fukwe za kuvutia, maji safi ya bluu, historia ya kuvutia, na tamaduni zinazojumuisha mchanganyiko wa kiarabu, kiafrika, kihindi, na kiswahili.

Wakati wa kipindi cha msimu wa utalii, watalii kutoka mataifa ya Ulaya kama Ujerumani, Ufaransa, Italia, na Uingereza hujitokeza kwa wingi ili kufurahia hali ya hewa ya joto na utulivu wa kisiwa. Wengi huja kuogelea, kufurahia matembezi ya baharini, na kujionea mandhari nzuri ya jua linapozama.

Watalii kutoka mataifa ya Afrika kama vile Afrika Kusini, Kenya, Uganda, na Nigeria wanajitokeza zaidi kutokana na urahisi wa usafiri ndani ya bara.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Mtakwimu Mkuu Zanzibar, jumla ya wageni walioingia Zanzibar mwezi Agosti, 2024 ni 72,296 ikilinganishwa na idadi ya wageni 61,466 ambao waliingia mwezi Agosti mwaka jana sawa na ongezeko la asilimia 17.6 huku bara lililoomgoza kwa wageni wengi zaidi likiwa ni bara la Ulaya.

Haya ni mabara yaliyoongoza kutembelea Zanzibar mwezi Agosti, kwa mujibu wa Ofisi ya Mtakwimu Mkuu Zanzibar;

1. Ulaya: 48,879
2. Afrika: 10,321
3. Asia: 7,700
4. Amerika: 4,586
5. Oceania: 778

Send this to a friend