Mabehewa 6 yaanguka Tabora

0
26

Mabehewa sita ya treni ya abiria iliyokuwa ikitoka Kigoma kwenda Dar es Salaam yameanguka mkoani Tabora, kata ya Malolo.

Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora ACP. Richard Abwao amesema kuhusu majeruhi na vifo bado jeshi la Polisi linaendelea kufuatilia kutokana na abiria wengi kukimbizwa katika hospitali ya Mkoa wa Tabora Kitete kwa ajili ya matibabu.

Aidha amesema chanzo cha ajali hiyo mpaka Sasa bado hakijajulikana na ufuatiliaji bado unaendelea.

Send this to a friend