Mabenki yaungana pamoja kujadili Ujumuishi Sekta ya Fedha

0
34

Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA) umefanya Kongamano la Pili la ujumuishi wa Kifedha ambalo limewaleta wadau katika sekta ya fedha pamoja kujadili fursa, changamoto na namna ya kuwafanya watanzania wengi watumie huduma za kifedha hususani zile za kibenki

Pamoja na kongamano hilo TBA imezindua Kanuni za Usimamizi Endelevu wa Sekta ya Fedha.

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Emmanuel Tutuba (wa tatu kushoto mbele) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mabenki na viongozi wa taasisi mbali mbali muda mfupi baada ya kufungua mkutano wa Pili wa Ujumuishi wa Kifedha ulioandaliwa na Umoja wa Mabenki Tanzania na kufanyikia jijini Dar es Salaam.

Akiongea wakati kongamano hilo, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Emmanuel Tutuba aliyekuwa mgeni rasmi aliyapongeza mabenki kwa kuja na kanuni ambazo pamoja na mambo mengine alisema utakuwa na mchango mkubwa katika kuongeza ujumifu kwenye sekta ya fedha.

Gavana Tutuba alisema kanuni hizi zitaweza kuongeza ujumuishi haswa kwa makundi ambayo yamekuwa yakianchwa nyuma na hivyo kuongeza idadi ya Watanzania ambao wapo kwenye mfumo rasmi wa kifedha.

“Tangu tumezindua Mpango wa Tatu Jumuifu wa Sekta ya Fedha tumeweza kufikia asilia 76 lakini lengo letu ni kufikia aslimia 85 kufikia mwaka 2028. Kanuni hizi zitayasaidia mabenki na taasisi za kifedha kutelekeza majukumu yao na kuyagusa makundi ambayo yameanchwa nyuma,” alisema

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Emmanuel Tutuba akihutubia wakati wa mkutano wa Pili wa Ujumuishi wa Kifedha ulioandaliwa na Umoja wa Mabenki Tanzania na kufanyika jijini Dar es Salaam

Gavana aliyahakikishaia mabenki ushirikiano kuwa Benki Kuu itaendelea kuwa mstari wa mbele kufanya kazi nayo na kutengeneza mazingira rafiki kwa mabenki kufanya shughuli zake.

Mwenyekiti wa TBA Theobald Sabi alisema mabenki yanafahamu uwepo wa makundi ikiwa ni pamoja na wanawake, vijana pamoja na watu wenye ulemavu ambao wameachwa nyuma kwenye huduma na za kifedha na kusema mkutano huo utajadili namna bora ya kuyajumisha.

Baadhi ya wageni waalikwa na wanachama wa Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA) wakifuatilia kwa makini hotuba ya Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Emmanuel Tutuba wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Pili wa Ujumuishi wa Kifedha uilioandaliwa na Umoja huo na kufanyika jijini Dar es Salaam.

“Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknalojia tunaamini kuwa sisi sekta ya benki tunaweza kuyafikia makundi maalum ambayo hayajafikiwa bado na kwa gharama nafuu,” alisema.

Katika kongamano hilo, Gavana pia amezindua Kanuni za Utumiaji Fedha endelevu (Sustainable Finance Principles (SFPs) zilizotengenezwa na TBA kwa kushirikiana na washirika wake BOT, WWF, IUCN & CEOrt

Mwenyekiti wa Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA) Theobald Sabi (kati kati) akibadilishana mawazo na baadhi ya wanachama na wageni waalikwa muda mfupi kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Pili wa Ujumuishi wa Kifedha uliofanyika jiijini Dar es Salaam. Mkutano huo umeandaliwa na TBA na ulifunguliwa na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Emmanuel Tutuba

Send this to a friend