Mabondia Hassan Mwakinyo na Ibrahim Class wavuliwa ubingwa wa WBF

0
60

Mabondia bora nchini Tanzania, Hassan Mwakinyo na Ibrahim Class wamevuliwa ubingwa wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa la Dunia (WBF).

Taarifa za shirikisho hilo imeeleza kuwa wapiga vitasa hao si mabingwa tena kwenye uzani wa kila mmoja.

Uamuzi wa kuwavua ubingwa umetokana na mabondia hao kushindwa kutetea ubingwa wao kwa wakati kama ambavyo kanuni za shirikisho hilo zinavyotaka.

Class ambaye ni bondia namba moja kwenye uzani wa Super Feather alitwaa mkanda wa ubingwa wa mabara wa WBF kwenye uzani wa light Januari 29, 2021 baada ya kumchapa Denis Mwale kwa pointi.

Kwa upande wake Mwakinyo ambaye ni namba moja kwenye uzani wa Super Welter Afrika alifanikiwa kutetea ubingwa wa uzani huo Novemba 12, 2020 baada ya kumshushia kipigo Jose Carlos Paz kwa TKO.

Katibu Mkuu wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC), Yahya Poli amesema taarifa za Mwakinyo ni za kweli na sasa ubingwa huo unashikiliwa na Victor Lonescu wa Romania.

Hata hivyo Poli amesema bado hawana taarifa za Class.

Send this to a friend