Maboresho ya mitambo kusababisha upungufu/katizo la umeme

0
52

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Maharage Chande ametangaza kuwepo kwa mgao wa umeme utakaoanza Februari Mosi hadi Februari 10 mwaka huu katika baadhi ya maeneo nchini.

Akizungumza na waandishi wa babari leo, ameeleza kwamba kumekuwa na miundombinu chakavu ambayo imekuwa ikisababisha kukatika kwa umeme mara kwa mara, hivyo watatumia siku 10 kufanya matengenezo katika mitambo ya kuzalisha na ya kusambaza umeme.

“Kutakuwa na athari kwenye baadhi ya maeneo. Tutatoa ratiba kwenye yale maeneo yatakayoathirika kuanzia kesho na kuendelea mpaka tarehe 10, ili wananchi na viwanda waweze kujipanga,” amesema.

Kwa upande wake Kaimu Meneja Kanda ya Mashariki, Mhandisi Kenneth Gwamanda ameongeza kuwa kutakuwa na upungufu wa uzalishaji wa umeme kutokana na matengenezo katika mfumo wa gesi.

Matengenezo hayo yamewekwa katika makundi mawili ambayo yanahusisha maeneo yenye changamoto kubwa, na maeneo yenye athari ndogo.

Send this to a friend