Machangudoa Mombasa wagoma kutoa huduma kwa madereva bodaboda

1
74

Wanawake wanaofanya biashara ya kuuza miili yao mjini Mombasa wameungana na wenzao nchini Kenya kulaani vitendo vya udhalilishaji wa kingono vilivyofanywa kwa dereva bodaboda mwanamke jijini Nairobi.

Wanawake hao kupitia chama chao wamesema kuonesha mshikamano na madereva bodaboda wanawake nchini humo hawatatoa huduma ya ngono kwa kwa madereva bodaboda wanaume kwa wiki moja ijayo.

“Hawa watu ni wateja wetu, lakini kuanzia leo, hakuna mwanamke anayejiuza aliyesajiliwa akatayetoa huduma ya ngono kwa dereva yeyote wa bodaboda kwenye eneo hili. Endapo mmoja wetu akikutwa na dereva bodaboda kwa kipindi tajwa, atafutiwa usajili wake,” chama cha wanawake hao kimeeleza.

Wamesema kuwanyima huduma madereva hao ni moja ya njia ya kushinikiza haki kwa wanawake ambao wamekuwa wakikumbana na madhali ya unyanyasaji kwenye maeneo ya umma.

“Tunajua kwamba hapa ndio tunapata mahitaji yetu ya msingi na kuhudumia familia zetu, lakini tupo tayari kushinda njaa ili vitendo kama hivyo vikomeshwe,” wamesisitiza.