Machinga, bodaboda wamwagia sifa uongozi wa Rais Samia

0
43

Shirikisho la vyama vya madereva wa pikipiki, bajaji na wamachinga wa Mkoa wa Dar es Salaam wameunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan hasa katika kuinua uchumi wa taifa.

Akizungumza Mwenyekiti wa Wamachinga, Namoto Yusuph amesema wanampongeza Rais Samia kwa kuleta maridhiano ya kisiasa na kuruhusu mikutano ya kisiasa, ubunifu wa filamu ya Royal Tour uliokuza sekta ya utalii pamoja na kufungulia vyombo vya Habari vilivyokuwa vimefungwa.

“Tunatambua mchango wa Rais Samia kwa kutambua kundi la wamachinga kama kundi muhimu kwa kutumia TZS milioni 10 kwa kila mkoa kujenga ofisi za wamachinga na kwa mara ya kwanza amelitambua kundi hili pamoja na kutuwezesha sisi bodaboda na wamachinga kwenda Uganda kupata mafunzo ya ujasiriamali,” amesema.

Kinana: Wapinzani jengeni hoja na si kumkejeli Rais Samia 

Ameongeza “Sisi bodaboda, bajaji na wamachinga tunaunga mkono mpango wa uwekezaji katika Bandari ya Dar es Salaam kwani tunaamini kuwa shughuli za bandari zikiboreshwa bidhaa zetu zitaimarika na bei za bidhaa zitashuka, bei za bandari zitapungua kutokana na ubora wa gharama za forodha kuimarika.”

Aidha, Katibu wa shirikisho hilo, Michael Riganya amempongeza Rais kwa kuwapunguzia tozo za pikipiki kutoka TZS 180,000 hadi 120,000 punguzo la faini kutoka 30,000 hadi 10,000.