Madagascar hatarini kuelemewa na wagonjwa wa corona

0
39

Maafisa kutoka katika baadhi ya hospitali jijini Antananarivo, Madagascar wametahadharisha kuwa huenda maeneo ya kutoa huduma yakaelemewa na wagonjwa kutokana na kuongezeka kwa kasi ya maambukizi ya virusi vya corona.

Moja ya hospitali nchini humo imeeleza kuwa ina uwezo wa kuhudumia wagonjwa 50 na tayari wana wagonjwa 46 hivyo kumebaki nafasi ya wagonjwa wanne tu.

Waziri wa Afya wa Madagascar ameandika barua kwenda kwa wakala wa misaada wakiomba kupatiwa misaada ya vipimo, mashine za kupumulia na vifaa kinga kwa ajili ya watoa huduma ili kusaidia mapambano dhidi ya virusi hivyo.

Muwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini humo ametahadharisha kuwa kwa hali ilivyo hospitali zitakuwa na wagonjwa wengi kabla ya kasi ya maambukizi haijafika kileleni.

Zaidi ya visa 7,500 vya maambukizi ya COVID-19 vimeripotiwa nchini humo ambapo zaidi ya 80% ya visa hivyo vimetokea mwezi uliopita.

Katika hatua nyingine kuhusu hali ya virusi hivyo barani Afrika, Rais wa Liberia, George Weah ameondoa hali ya hatari iliyotangazwa Aprili 2020 kwa lengo la kupambana na virusi hivyo na ameagiza wanajeshi waliokuwa mitaani kutekeleza amri hiyo warudi kwenye kambi zao.

Kwingineko nchini Afrika Kusini, watengenezaji wa vilevi (wine) wameandamana mitaani wakiwa na chupa tu, hatua ambayo imekuja kufuatia serikali kurejesha zuio la kutoka nje na matumizi ya pombe.

Send this to a friend