Madagascar: Maseneta wawili wafariki kwa corona, 25 wakutwa na maambukizi

0
44

Watunga sheria wawili, seneta mmoja na naibu seneta mmoja wamefariki dunia kutokana na maambukizi ya virusi vya corona, Rais wa Madagascar Andry Rajoelina ametangaza.

Rais huyo ameongeza pia kuwa maseneta wengine 14 na naibu 11 wamekutwa na maambukizi ya virusi hivyo vinavyoendelea kugharimu maisha ya watu duniani.

Hivi karibuni serikali ya nchi hiyo ilirudisha baadhi ya hatua ilizokuwa imechukua kukabiliana na corona ikiwa ni pamoja na kuufunga Mji Mkuu, Antananarivo kutokana na kuanza kuongezeka kwa kasi ya maambukizi mapya.

Zaidi ya visa 3,570 vimeripotiwa nchini humo na watu 34 wamefariki dunia tangu kisa cha kwanza kiliporipotiwa nchini humo Machi mwaka huu.

Send this to a friend