Madagascar yapitisha sheria ya kuwahasi wabakaji wa watoto

0
46

Bunge la Madagascar limeidhinisha sheria mpya ambayo itawafanya watu waliopatikana na hatia ya unyanyasaji wa kingono kwa watoto kuhasiwa na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela.

Kwa mujibu wa sheria mpya, wanaopatikana na hatia ya kubaka watoto wenye umri kati ya miaka 10 hadi 13, watahasiwa kwa kemikali na kifungo cha miaka 15 hadi 20 pamoja na kazi ngumu, lakini ikiwa mkosaji ni mdogo, hatapata adhabu ya kuondolewa kiungo chake.

Hayo yamejiri siku chache baada ya Kazakhstan kuwasilisha sheria sawa na hiyo kutokana na wabunge wa eneo hilo kushutumu kuwa kuhasiwa kwa kemikali, adhabu iliyotolewa kwa wabakaji kwa watoto, kumeshindwa kukomesha watu kufanya uhalifu huo.

Miji 10 Afrika yenye kiwango kikubwa cha uhalifu

Awali, wabakaji wa watoto nchini Madagascar walihukumiwa kifungo cha miaka mitano hadi 20 pamoja na kazi ngumu.

Hata hivyo, hatua hiyo imepingwa na Mkurugenzi wa Kikanda wa Amnesty International kwa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika, Tigere Chagutah ambaye amesisitiza kuwa adhabu ya kuhasiwa kwa kemikali na upasuaji ni ukatili, unyama na mateso yasiyofaa kwa mujibu wa viwango vya haki za binadamu vya kikanda na kimataifa.

Send this to a friend