Madaktari bingwa wafanikiwa kuziba mfuko wa chakula wenye matundu mengi

0
72

Madaktari Bingwa na Ubingwa Bobezi wamefanikiwa kufanya upasuaji kwa mwanaume mwenye umri wa miaka (41) mkazi wa Wilaya ya Nachingwea na kufanikiwa kuziba mfuko wake wa chakula uliokuwa na matundu mengi.

Hayo yameelezwa na Mganga Mfawidhi Hospitali ya Wilaya ya Nachingwea, Dkt. Shukrani Nsikini ambaye ameeleza kuwa upasuaji huo umefanyika Septemba 18,2024 katika Hospitali ya Wilaya ya Nachingwea ukiongozwa na Daktari Bingwa Norbet Njee kutoka hospitali wa Kanda ya Ligula Mtwara akishirikiana na Dkt. Rajab Sadiki wa Hospitali ya wilaya ya Nachingwea.

“Tulipata mgonjwa mwanaume ambaye alikuwa anaeleza kuwa anaumwa tumbo na anakosa choo, lakini baadae akawa anapata choo kidogo kisha maumivu makali na tumbo kuvimba, Daktari bingwa alipo muangalia akasema anahitaji upasuaji,” amesema Dkt. Nsikini.

Ameongeza kuwa baada ya kumfanyia upasuaji waligundua kwamba mfuko wa chakula ulikuwa na matundu mengi na kupelekea chakula kuvujia tumboni na kusababisha mgonjwa kukosa nguvu kabisa.

Dkt. Nsikini amesema upasuaji huo umekuwa wa mafanikio na mgonjwa ameamka, na sasa anaendeelea na mazoezi madogomadogo.

Send this to a friend