Madaktari wamshukuru Rais Samia kwa mazingira mazuri ya kazi

0
43

Madaktari kutoka Kanda ya Ziwa wameipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira rafiki na mazuri ili kuhakikisha Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) unatekeleza malengo yake ya ulipaji wa fidia kwa wafanyakazi wanaoumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi.

Wameyasema hayo jijini Mwanza mwishoni mwa kikao kazi kilichoandaliwa na WCF kuwajengea uelewa madaktari kutoka mikoa ya Kanda ya ziwa kuhusu namna ya kufanya tathmini ya ulemavu na magonjwa yatokanayo na kazi.

“Napenda kuishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuweka mazingira rafiki na mazuri kuhakikisha WCF inaweza kutekeleza malengo yake kwa maana ya kuhudumia watumishi wa sekta ya umma na sekta binafsi wanaoumia au kuugua kutokana na kazi.” amesema Dkt. Pasclates Ijumba kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita.

Rais Samia: Ni fahari Watanzania tumejenga Ikulu yetu

Amesema mafunzo hayo yamewawezesha kuelewa kuwa madaktari wanahusika katika mchakato wa kusaidia WCF kulipa fidia stahiki kwa kufanya tathmini sahihi.

Naye Dkt. Noel Saitoti kutoka Hospitali ya Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera amesema licha ya ukweli kwamba WCF ina muda mfupi wa miaka minane tangu kuanzishwa kwake, imekuwa ni mfano wa kuigwa kutokana na mifumo yake mizuri ya utoaji huduma na kuzipita nchi nyingi za Afrika zilizotangulia muda mrefu kwenye sekta ya utoaji fidia kwa wafanyakazi.

Ameeleza kuwa mafanikio hayo yametokana na serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wake Rais Samia ambaye kupitia Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu inayosimamia mfuko huo imeuwezesha kutekeleza vema majukumu yake.

Send this to a friend