Madaktari waomba wanaojaribu kujiua wasishtakiwe

0
55

Madaktari wanaoratibu magonjwa ya afya ya akili wameiomba Serikali kupitia upya sheria ya kuwafunga watu wanaofanya jaribio la kujiua ili wapatiwe tiba na kuondokana na tatizo hilo katika jamii.

Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Huduma ya Ubora wa Hospitali ya Taifa ya Magonjwa ya Akili Mirembe, Dkt. Minael Urio amesema waathirika hao wanapaswa kupelekwa hospitalini kupatiwa mtibabu ili kubaini tatizo linalowasumbua mpaka kufikia hatua ya kutaka kujiua.

“Wakipata nafasi ya kutibiwa inaweza kusaidia kumtoa katika hatua aliyofikia badala ya kubaki vivyo hivyo akiwa mahabusu. Tunaomba sheria iangaliwe upya ili kuwanusuru waathirika wa matukio haya nchini,” ameshauri Dkt. Urio.

Ameongeza, ulimwenguni takribani watu 800,000 hujiua kila mwaka kutokana na sababu mbalimbali na kila baada ya sekunde 40 watu hufanya jaribio la kujiua.”

Chanzo: Nipashe

Send this to a friend