Madam Ritta apewa siku 30 amlipe mshindi wa BSS 2019

0
40

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza ametoa mwezi mmoja kwa uongozi wa Kampuni ya  Benchmark Production inayoendesha mashindano ya kusaka vipaji kwa wasanii wa muziki (Bongo Star Search-BSS) kumlipa mshindi  wa kwanza wa mwaka 2019,  Meshack Fukuta zawadi yake TZS 50 milioni.

Shonza ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwa lengo la kueleza umma jitihada ambazo serikali imefanya baada ya kupokea barua ya malalamiko ya kuto kulipwa kwa mshindi huyo kutoka kwa familia yao.

Fainali za 10 za mashindano ya hayo nchini Tanzania zilifanyika usiku wa kuamkia Jumatano Desemba 25, 2019 ambapo Meshack Fukuta kutoka mkoani Mbeya aliibuka mshindi baada ya kuwa ameshiriki mara tatu pasina kushinda.

Mbali na kiasi hicho cha fedha alichoahidiwa kama mshindi wa kwanza, alipewa ofa ya kusimamiwa muziki wake kwa mwaka mzima ambapo pia atakuwa na meneja.

Send this to a friend