Madanguro 324 yapo kwenye makazi ya watu Kinondoni

0
40

Mstahiki Meya wa Kinondoni, Songoro Mnyonge amewataka wamiliki wa nyumba zilizogeuzwa madanguro wajisalimishe ambapo amedai kwa Mwananyamala, Msasani na Uwanja wa Fisi pekee kuna madanguro 324.

Akizungumza kuhusu kutokomeza madanguro ndani ya Manispaa ya Kinondoni, amesema wamebaini madanguro hayo yapo maeneo ya makazi ya watu, na kwamba wanaojihusisha na biashara hizo ‘madada poa’ hujiuza hadharani wakati wa mchana kitendo kinachoweza kuchangia ongezeko la maambukizi ya UKIMWI.

“Nilishtukiza Mwananyamala kuna madanguro 150, yapo watu wamegeuza nyumba zao kuwa za biashara za wadada kuuza miili yao, Uwanja wa Fisi (Tandale) yapo 139, Msasani yapo 35 kwa hiyo madanguro jumla 324 kwa maeneo hayo pekee,” amesema.

Mahakama yavunja ndoa ya Kafulila na Jesca, suala la watoto laamuliwa

Mnyonge amedai katika harakati hizo wamebaini kuwa madada poa hao huchangishana fedha na kuwahonga baadhi ya viongozi ili wasiwazuie kufanya biashara huku akiahidi kuwa endapo viongozi hao watabainika watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Aidha, amemuomba Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum, Dkt. Dorothy Gwajima kuweka nguvu katika kukomesha Madanguro ili kuweza kuzuia na kutokomeza kabisa biashara hizo.

Send this to a friend