Madaraja 10 marefu zaidi barani Afrika

0
109

Madaraja ni moja kati ya kipengele muhimu kwenye miundombinu ya kisasa. Madaraja huunganisha miji, visiwa na kutumika kama sehemu ya kuvusha katika maeneo mbalimbali.

Hii ni orodha ya madaraja marefu zaidi na ya kipekee barani Afrika ambayo yamegeuka kivutio kwa watu wengi;

1.        6 Oktoba Bridge, Misri – Maili 12.7  (20.5 Km)

Daraja la Oktoba 6 nchini Misri ndilo refu zaidi barani Afrika. Daraja hili lilijengwa kuunganisha mji mkuu wa Cairo. Wataalam wanakadiria kuwa watu 500,000 hutumia daraja hilo kila siku kwenda kazini, uwanja wa ndege au miji mingine. Wenyeji wameupa jina la utani la ‘uti wa mgongo wa Cairo.’

2.        Daraja la Third Mainland, Nigeria – Maili 7.3 (Km 11.8)

Daraja hilo lililopewa jina la Rais Ibrahim Babangida, lina urefu wa maili 7.3 na kulifanya kuwa daraja la pili kwa urefu barani Afrika. Limejengwa mwishoni mwa miaka ya 1970 ili kupunguza msongamano huko Lagos.

3.        Suez Canal Bridge, Misri – Maili 2.4 (Km 3.9)

Japan na Misri zilitoa msaada wa kifedha ili kujenga daraja hilo kama sehemu ya harakati ya kuendeleza maeneo yanayozunguka Mfereji wa Suez. Ujenzi ulianza mwaka wa 1995, ulichukuwa miaka sita na daraja lilifunguliwa Oktoba 9, 2009.

4. Daraja la Kisiwa cha Msumbiji, Msumbiji – Maili 1.9 (Km 3.8)

Tofauti na madaraja mengine mengi kwenye orodha hii, Daraja la Kisiwa cha Msumbiji halipiti kwenye mto badala yake ni kwenye bahari ya Hindi ili kuunganisha Kisiwa cha Msumbiji. Lilijengwa mnamo mwaka 1969.

5. Daraja la Dona Ana, Msumbiji – Maili 2.3 (Km 3.67)

Kaptour 2005

Wareno walijenga daraja hili kwa usafiri wa reli mnamo mwaka 1934. Baadaye lilifungwa kwa takribani miaka kumi na kisha kufunguliwa mwaka 1980. Mwaka 2009 na 2016, lilirekebishwa ili kutumika kama njia ya reli na watembea kwa miguu. Sasa linapitisha watembea kwa miguu zaidi ya 3,000 kwa siku.

6. Daraja la Armando Emilio Guebuza, Msumbiji – Maili 1.5 (Km 2.37)

Daraja hili lililopewa jina la Armando Guebuza, Rais wa zamani wa Msumbiji, linaunganisha majimbo ya Sofala na Zambezia. Lilijengwa mwishoni mwa miaka ya 2000 kuchukua nafasi ya vivuko likichukua miaka minne na dola za Marekani milioni 72 kukamilika na hatimaye kuzinduliwa Agosti 1, 2009.

7. Daraja la Qasr Al-Nil, Misri – Maili 1.2 (Km 1.93)

Daraja la Qasr Al-Nil ni mojawapo ya madaraja maarufu zaidi ya Misri lililojengwa kuchukua nafasi ya daraja la kwanza lililopita Mto Nile, Qasr Al-Nil. Daraja hilo lenye umri wa miaka 90 ni mojawapo ya miundo ya kuvutia sana nchini Misri.

8. Daraja la Wouri, Cameroon – Maili 1.1 (Km 1.8)

Wafaransa waliijenga daraja hili katika miaka ya 1950 enzi ya ukoloni ili kuunganisha bandari ya Bonaberi hadi Douala. Pamoja na kuwa moja ya madaraja marefu zaidi, Daraja la Wouri pia ni mojawapo ya madaraja kongwe zaidi.

9. Daraja la Mkapa, Tanzania – Maili 0.6 (970 M)

Daraja hili lililopewa jina la Benjamin Mkapa, Rais wa Tatu wa Tanzania, lilibuniwa na H. P. Gauff Ingenieure GmbH & Co na kujengwa na kampuni ya Italia juu ya Mto Rufiji. Lilizinduliwa mwaka 2003 likiwa na urefu wa wa maili 0.6, na kulifanya kuwa mojawapo ya madaraja marefu zaidi ya barabara barani Afrika.

10. Daraja la Katima Mulilo, Namibia – Maili 0.56 (900 M)

Daraja hili pia linajulikana kama Bridge 508, ni daraja la urefu wa maili 0.56 huko Katima Mulilo, Namibia na Shesheke, Zambia. Ilifunguliwa rasmi mwaka 2004 na Marais wa nchi zote mbili. Katima Mulilo limekuwa likisaidia biashara ya Namibia na Zambia kwa miongo miwili.