Madareva wafungiwa leseni zao

0
38

Kikosi ch Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kimewakamata jumla ya madereva 13 kwa makosa ya uvunjifu wa sheria za usalama barabarani, na watano kati yao wamefungiwa leseni zao.

Taarifa ya polisi inaeleza kuwa madereva hao wamekamatwa kwa makosa mbalimbali yakiwemo mwendokasi, na kupita magari mengine bila kuchukua tahadhari (overtaking).

Aidha, watuhumiwa watano wa makosa ya usalama barabarani wamefikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili, huku wengine nane majalada yao yamepelekwa ofisi ya Taifa ya mashtaka kwa hatua zaidi za kisheria.

Jeshi la Polisi limewaomba wananchi kutoa taarifa za madereva wanaovunja sheria za usalama barabarani ili hatua kali zichukuliwe dhidi yao kwani kwa kufanya hivyo kutaepusha ajali zinazoweza kuepukika, na kunusuru maisha ya watu na mali zao.

Send this to a friend