Madee atozwa faini, wimbo wafungiwa na BASATA

0
97

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limemtoza faini ya TZS milioni 3 mwanamuziki Madee pamoja na kumfungia kujishughulisha na kazi za sanaa mpaka hapo atakapolipa faini hiyo kwa kosa la kuchapisha wimbo unaokiuka maudhui ya BASATA.

Aidha, limemtoza faini ya TZS milioni 1 mtozi (producer) Mr. T Touch pamoja na kumwamuru msanii huyo kuutoa wimbo huo kwenye majukwaa ya kidijitali.

Vilevile, BASATA imemtoza faini ya milioni 1 mhusika aliyepandisha wimbo huo kwenye majukwaa ya kidijitali.

“Baraza linawasihi wasanii kuongeza ubunifu wanapozalisha kazi zao za Sanaa, hata hivyo linawakumbusha kuzingatia mwongozo wa maadili katika kazi za sana unaopatikana katika tovuti za BASATA,” imeeleza taarifa ya BASATA

Send this to a friend