Madereva kutoka nchini Kenya wanalazimika kukimbilia nchini Tanzania kununua mafuta ya petroli na dizeli kutokana na unafuu uliopo nchini ukilinganishwa na bei ya Kenya.
Madereva hao wa malori na magari ya umma na binafsi, wamevuka mpaka wa Namanga huku wafanyabiashara wa Kenya wanaouza mafuta katika eneo hilo wakilalamika kupungua kwa biashara kutokana na kuongezeka kwa gharama ya mafuta nchini humo.
Katika mpaka wa Namanga bei ya petroli kwa Tanzania ni inauzwa TZS 3,297 na dizeli ikiuzwa TZS 3,343 huku bei ya petroli na dizeli kwa Kenya ikiuzwa zaidi ya 3,400.
“Hata watu wa pikipiki wote wanakuja huko Tanzania. Tunaiomba Serikali itupunguzie gharama kidogo angalau maana watu wengi pesa wanapeleka Tanzania,” amesema mmoja wa wafanyabiashara wa mafuta katika mpaka wa Namanga.
Aidha, wauzaji hao wameshangazwa na unafuu wa bei za mafuta nchini Tanzania licha ya tatizo hilo kuwa janga la kidunia.