Madereva Kenya wakimbilia Tanzania kununua mafuta kwa bei nafuu

0
13

Maelfu ya wamiliki wa magari pamoja na waendesha boda boda katika mji wa mpakani wa Namanga wanaendelea kuingia nchini Tanzania ili kununua mafuta kwa bei rahisi.

Hivi karibuni shirika la kudhibiti bei ya mafuta nchini Kenya (EPRA) liliongeza bei ya mafuta kwa mujibu wa sheria ya fedha ya 2023, ambayo VAT iliongezeka kutoka asilimia 8 hadi asillimia 16.

Baadhi ya maeneo nchini Kenya ikiwemo mji wa Nairobi lita moja ya petroli inauzwa kwa shilingi 195.5 za Kenya [TZS 3,382] huku nchini Tanzania ikiuzwa kwa shilingi 2,781 za Tanzania ambazo ni shilingi 160 za Kenya.

Serikali Zanzibar yatoa ufafanuzi suala la wanaume kusuka

Kulingana na uchunguzi uliofanywa na gazeti la Nation Media, bei ya mafuta imekuwa ikishuka nchini Tanzania katika kipindi cha miezi miwili iliyopita huku ikipanda nchini Kenya.

Send this to a friend