Madereva wa mabasi ya shule wadaiwa kubaka, kunajisi watoto

0
41

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe amesema amepokea malalamiko mengi kutoka kwa wazazi na walezi, wakidai watoto wao kufanyiwa vitendo vya ubakaji katika magari ya shule.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam katika mkutano wa Maofisa Ustawi wa Jamii na kuwataka wazazi na walezi kuwa makini kufuatilia taarifa za watoto wao pamoja na kujenga ukaribu ili wanapokumbana na changamoto waseme haraka.

Watoto wafariki baada ya wazazi kuwapakwa kinyesi kukausha vitovu

Aidha, kutokana na matukio mengi kuripotiwa, Wilaya ya Kinondoni imeanzisha utaratibu wa kuweka Matron katika gari za kubeba wanafunzi ili kuzuia vitendo hivyo vinavyodaiwa kufanywa na madereva wa magari hayo.

“Kesi ziko nyingi watoto kufanyiwa ukatili kwenye School Bus, tusiwaamini sana hiyo ni changmoto, kwenye mabasi Kinondoni tumesema lazima awepo matron na tumepitisha hiyo sheria,” amesisitiza.

Send this to a friend