Madhara 5 ya kutumia choo cha kukaa

0
95

Mtu anapotumia choo cha kukaa njia yake ya kihifadhi kinyesi huwa imebanwa kiasi, hivyo hatoi kinyesi chote wakati wa kujisadia. Hali hii huchangiwa kutokujikunja vya kutosha na kuweka presha kwenye mfuko huo.

Misuli inayoshikiria kihifadhi kinyesi huwa imelegezwa nusu ya jinsi inavotakiwa iwe imelegezwa. Lakini mtu anapochuchumaa, huruhusu misuli kulegea vya kutosha na kurahisisha kinyesi chote kutoka nje na kukidhi haja nzima.

Yafuatayo ni matokeo ya kutumia choo cha kukaa

Bawasiri
Ni ugonjwa unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu ya ndani na nje ya sehemu ya haja kubwa kutokana na mishipa kubanwa kwa mda mrefu na kinyesi ambacho mara nyingi huwa ni matokeo ya kutomaliza haja au kubana kwenda mapema haja. Madhara yake wakati mwingine mishipa hiyo huweza kupasuka na kuvuja damu kwenye njia ya haja kubwa na kusababisha kutoka kinyama au uvimbe.

Saratani ya utumbo mpana
Mtu mwenye bawasiri mara nyingi hua kwenye hatari ya kupatwa na saratani ya utumbo mpana japo sababu nyingine hua ni kurundikana kwa kinyesi muda mrefu, jambo ambalo husababisha kinyesi hicho kugeuka sumu na hivyo kusababisha madhara kwenye utumbo mpana. Madhara haya yanaweza kukua mpaka kuwa saratani endapo hayatatafutiwa tiba haraka.

Daktari: Mtu mmoja anatakiwa kufanya ngono mara tatu kwa wiki

Kupata shida ya haja ndogo kwa wanawake
Maumbile ya mwanamke yameumbwa kufanya kazi vizuri wakati akiwa kwenye mkao wa kuchuchumaa wakati wa haja zote mbili. Choo cha kukaa huleta madhara ya kukosa kukojoa mkojo wote na hivyo inaweza kusababisha madhara kwenye kibofu cha mkojo.

Kukosa choo
Mtu anayetumia choo cha kukaa mara nyingi hua hamalizi haja na mrundikano wa haja ufanya kinyesi kuwa kigumu na kupelekea mtu kupata choo kigumu atakapojisadia wakati mwingine.

Maagonjwa ya ngozi
Vyoo vya kukaa huweza kuambukiza magonjwa ya ngozi kwenye makalio endapo vitatumika sehemu za umma ambako kusimamia usafi wa vyoo hivyo huwa mdogo.

Send this to a friend