Wafanyakazi wanaokaa kwa muda mrefu kwenye viti wameshauriwa kujenga tabia ya kusimaa na kufanya mazoezi ya kunyoosha mwili ili kuondokana na hatari ya kuvimba miguu kutokana na kubana kwa mishipa ya damu.
Hayo yamezungumzwa na Mtaalamu wa Udhibiti wa Magonjwa wa Wizara ya Afya, Dkt. Baraka Nzobo ambapo amewashauri wafanyakazi hususani makatibu mahsusi ambao wanakaa kwa muda mrefu kutenga muda kidogo wa kutembea ili kuipa nafasi mishipa ya damu kufanya kazi vizuri.
“Kiafya si vyema mtu kukaa chini zaidi ya saa tatu, unapaswa kusimama na kutembea ili kuipa nafasi mishipa ya damu kufanya kazi yake vizuri ya kusambaza damu na kuepusha tatizo la kuvimbaa miguu,” amesema Nzobo.
Mambo matatu ya kufanya unapozimikiwa na gari njiani
Aidha, ameshauri kuwa mazoezi ya kufanya sio kukimbia pekee, bali kutembea pia ni mazoezi mazuri hususani kwa mtu ambaye hajawahi kufanya mazoezi.
Chanzo: Nipashe