Madhara yatokanayo na kutumia dawa za kuongeza nguvu za kiume

0
86

Upungufu wa nguvu za kiume ni hali ya sehemu za siri za mwanaume kuwa na uwezo mdogo au kutokuwa na uwezo kabisa kuhimili tendo la ndoa kwa muda mrefu.

Kutokana na tatizo hilo kuenea katika jamii, kumeibuka matumizi mabaya ya dawa za kuongeza nguvu za kiume pasipo kufuata ushauri wa wataalam wa afya, huku zikitajwa kuwa na madhara makubwa kwa watumiaji.

Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi wa Dawa wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Dkt. Yonah Mwalwisi amesema taarifa zisizo rasmi zinasema matumizi holela ya dawa hizo yamechangia uwepo wa madhara ya kiharusi, mshtuko wa moyo, kuzimia na hata kifo.

Amesema dawa hizo husababisha kusimama kwa sehemu za siri za mwanaume kwa muda mrefu, hali inayoweza kusababisha pia maumivu ya sehemu hizo kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa Dkt. Mwalwisi, tatizo hilo lisipodhibitiwa kwa haraka linaweza kuharibu mishipa laini iliyoko ndani ya sehemu hizo na kusababisha tatizo kubwa.

Madhara mengine yaliyotajwa kutokana na matumizi ya dawa hizo endapo zitatumika sambamba na dawa zinazotibu maumivu ya moyo, husababisha kupungua kwa kiasi kikubwa kwa shinikizo la damu na kupata kizunguzungu.

Chanzo: Habari leo

Send this to a friend