Madiwani Singida walia na ‘betting’ kuvunja ndoa za vijana

0
15

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida limeitaka Serikali kuchukua hatua za kudhibiti ongezeko la vijana wanaoshiriki michezo ya kubashiri kwa kuwa linasababisha ndoa nyingi kuvunjika.

Hayo yamesemwa wakati wakijadili kamati ya fedha na uchumi kwenye kikao cha baraza hilo cha robo tatu kilichofanyika mkoani humo kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu.

Akizungumza katika kikao hicho, Diwani wa Kata ya Mtunduru, Ramadhan Mpaki amesema kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na kasi kubwa ya ndoa kuvunjika kutokana na vijana wengi kujihusisha na michezo hiyo ya kubashiri ambayo inachezwa hadi usiku wa manane na hivyo kusababisha mizozo katika ndoa zao.

Mwanafunzi ajiua baada ya kuliwa ada ya chuo kwenye kamari

“Halmashauri yetu iangalie upya sheria ya mchezo huu wa kubashiri kwani pamoja na kuwa chanzo cha mapato vijana wamekuwa wakicheza mchezo huo hadi usiku wa maneno ambapo pia wamekuwa wakipanga vitendo vya uhalifu ikiwa ni pamoja na kutishia ndoa za watu,” amesema

Send this to a friend