Madiwani wamshitaki mkurugenzi kwa Waziri Mkuu kwa kununua gari la milioni 470

0
60

Baadhi ya madiwani wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam wamedai Sheria ya Manunuzi ya Umma haikuzingariwa wakati wa ununuzi wa gari la Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Lusubilo Mwakabibi.

Madiwani hao wamesema kuwa mkurugenzi huyo alitumia ubabe kuilazimika kamati ya zabuni kutekeleza matakwa yake kununua gari (Toyota Landcruser XVR), kwa gharama ya TZS milioni 470, huku manispaa ikikabiliwa na changamoto nyingi.

Hata hivyo, mkurugenzi huyo hakutaka kulizungumzia kwa kina suala hilo badala yake alikiri kuwa ni kweli wamenunua gari hilo.

“Ni kweli, tumenunua gari hilo, lakini sina majibu kuhusu hilo, mimi ni mtumishi, kuna mamlaka zinazoweza kutoa majibu kwa niaba yangu kuhusu suala hilo, asante,” amesema Mwakabibi.

Mbali na ununuzi wa gari, pia wamedai kuna ubabe unaotekelezwa na mkurugenzi huyo kwa watumishi wa idara ya mbalimbali ikiwano ile ya zabuni na manunuzi, matumizi ya hovyo ya fedha za umma kwa ajili ya ukarabati wa ofisi yake na thamani za ofisi hiyo.

Shutuma hizo zimekuja siku chache baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kutoa siku saba kwa halmashauri zilizonunua magari ya gharama kujieleza.

Madiwani hao wamemuomba Waziri Mkuu, kuchukulia hatua kali dhidi ,ya mambo yaliyotekelezwa na mkurugenzi huyo na wengine aliosaidiana nao, ili kuwa fundisho.

Send this to a friend