Maelekezo ya Rais Samia kwa Msajili wa Vyama vya Siasa

0
21

Rais Samia Suluhu Hassan amemuagiza Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi kuitisha kikao maalum cha Baraza la Vyama vya Siasa lengo likiwa kuwashirikisha wadau katika kutathmini utekelezaji wa mapendekezo ya Kikosi Kazi kilochokuwa kikiratibu maoni ya watu kuhusu demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini.

Rais Samia ametoa maelekezo hayo wakati wa kikao kilichofanyika Ikulu na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali kuhusu kuanza kwa mchakato wa Katiba mpya.

Kikao hicho kimejadili namna ya kushirikisha wadau mbalimbali hasa ushirikishwaji wa  wanachi katika mchakato huo kutoka pande zote mbili Tanzania Bara na Zanzibar.

Mbali na mchakato huo wa Katiba mpya,  masuala mengine yanayotarajiwa kushughulikiwa ni marekebisho ya sheria mbalimbali zinazohusiana na uchaguzi zikiwemo Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Sheria ya Vyama vya Siasa.