Maelekezo ya Serikali kwa watu ambao hawajahesabiwa hadi sasa

0
20

Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi 2022, Anne Makinda amesema endapo itatokea mtu hajahesabiwa hadi kufikia jioni ya leo Agosti 29, 2022 ambayo ni tarehe ya mwisho ya zoezi hilo, bado atakuwa na nafasi ya kuhesabiwa.

Ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema taarifa zilizokwisha kukusanywa zinaonesha kuwa bado kuna asilimia 6.55 ya kaya ambazo hazijahesabiwa.

“Katika kufanikisha hili, mwananchi unashauriwa uende moja kwa moja kwenye Ofisi za Serikali za Mitaa, onana na Mwenyekiti au Mtendaji wa Mtaa unaoishi na hakikisha unawaachia namba ya mawasiliano ili karani akufuate ulipo na kuanza kazi ya kukuhesabu.”

Ameongeza, “Ofisi ya Taifa ya Takwimu imeandaa namba maalumu za mawasiliano kwa ajili ya wananchi ambao hawajahesabiwa kupiga simu moja kwa moja makao makuu Dodoma ili utaratibu wa kupeleka karani eneo husika ufanyike kwa wakati, namba hizo ni 0753665491, 0764443873, 0626141515, 0784665404 na 0656279424,” amesisitiza Makinda.

Makinda asema namba hizo zitatumika ndani ya siku saba, ikiwa ni kuanzia Agosti 30, 2022 hadi Septemba 5 mwaka huuu.

Send this to a friend