Maelekezo ya TCU kwa waliotunukiwa shahada za heshima na vyuo vya nje ya nchi

0
42

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imesema kuwa shahada za heshima nchini Tanzania zinatolewa nana vyuo vikuu vinavyotambulika na vilivyoorodheshwa kwa mujibu wa vifungu vya Sheria ya Vyuo Vikuu (Cap. 346) ya sheria za Tanzania.

Pia, shahada za heshima zinazotolewa na vyuo vya kigeni nje ya Tanzania zinatambuliwa na TCU endapo tu taasisi zilizotoa zimesajiliwa na kutambuliwa na mamlaka husika katika nchi zilizopo.

Tofauti ya Shahada ya Udaktari wa Heshima na Shahada ya Udaktari wa Falsafa (PhD)

Tume hiyo imesisitiza kwamba vyuo vya kigeni vinavyotaka kufanya shughuli zake nchi Tanzania vinatakiwa kufuata sheria na kanuni na kwamba ni kosa kisheria kuendesha shughuli za chuo nchini Tanzania, ikiwemo kutunuku shahada na tuzo nyingine za kielimu bila idhini ya TCU.

TCU umewataka wananchi kujiridhisha na uhalali wa shughuli za chuo husika hapa nchini kabla ya kushirikiana nacho katika jambo lolote.

Waliokosa GPA ya 4.4 wazuiwa kuhudhuria mahafali

Taarifa ya TCU imekuja siku chache baada ya Mbunge wa Geita Mjini, Joseph Musukuma kutunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima katika Siasa na Uongozi kutoka Chuo cha Academy of Universal Global Peace.

Tovuti ya chuo hicho inaeleza kimesajiliwa India, Uingereza na Marekani, hata hivyo hakimo katika tovuti rasmi za taifa za vyuo vya Uingereza na Marekani.

Send this to a friend