Maendeleo ya teknolojia ya kidijitali na umuhimu wake kwenye kukuza uchumi Tanzania

0
42

Duniani kote suala la matumizi ya teknolojia ya kidijitali linakua kwa kasi kubwa sana na kwa kiasi fulani kunachagizwa na matumizi ya intaneti/data kupitia simu za mkononi.

Kwa mujibu wa Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Biashara na Maendeleo, matumizi ya data duniani kote yanatarajiwa kuongezeka kufikia ujazo wa 150,700GB kwa sekunde mwaka 2022. Ukuaji huo ni mkubwa sana ndani ya miaka michache ambapo mwaka 2017 ujazo ulikuwa 46,000BG kwa sekunde.

Sehemu ya mafanikio haya imechagizwa na matumizi ya data barani Afrika kwa mfano, katika mtandao mmoja utumiaji wa data umekua kwa asilimia 52 mwaka 2019.Takwimu hizi za karibuni zinaonesha habari njema kwa uchumi wa Tanzania.

Kwa mujibu wa ripoti ya Benki ya Dunia sekta ya dijitali nchini Tanzania ni moja ya kichochea kikubwa cha ukuaji wa uchumi. Pia, kuzidi kusambaa kwa matumizi ya intaneti kwenye simu na ubunifu wa teknolojia ni moja ya njia bora za kuhakikisha Tanzania inafikia maendeleo ya kijamii katika miaka ijayo.

Kwa mfano, Sekta ya mawasiliano ya simu imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na sekta ya afya nchini Tanzania kuja na njia ya ubunifu ambayo itarawarahisishia wazazi kusajili watoto wao wanapozaliwa. Huduma kama hizi zinaweka misingi kwa wazazi kuweza kupata huduma mbalimbali kama huduma za afya na programu za chanjo.

Miaka si mingi ijayo, usajili wa vizazi utawasaidia watu juu ya kile kinachofahamika kama utambuzi wa kidijitali ambao utawezesha watu kupata kazi pamoja na kulipa kodi kwa urahisi.

Tigo Tanzania- moja ya watoa huduma wakubwa wa mawasiliano ya simu imechangia sana katika utoaji wa huduma. Programu tumishi ya Tigo inawawezesha wazazi na wakunga kusajili taarifa za kuzaliwa kwa watoto wao kwa kutumia simu ya mkononi. Mbali na kutoa huduma kwa urahisi na uharaka kwa wateja wengine, programu hii inawezesha kuhakikisha watu wanaweza kunufaika kwa mambo yote ya kijamii miaka ijayo.

Ili kuzisaidia kampuni za mawasiliano ya simu kuendelea kuleta utofauti wa kibunifu ni vyema kutilia maanani mahitaji yao na kuwasaidia kukua zaidi. Hii itasaidia Watanzania kuendelea kupata huduma bora na za uhakika na kukuza uchumi wetu.

Send this to a friend