Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) imetangaza kukosekana kwa huduma ya maji kwa wateja wanaotumia mtambo wa kuzalisha maji wa Ruvu Juu kwa wastani wa saa 16 siku ya Jumamosi.
Katika taarifa iliyotolewa leo na kitengo cha mawasiliano DAWASA imeeleza kuwa katizo hilo la maji litaanza kesho saa 12 jioni hadi siku ya Jumapili saa 4 asubuhi ilil kuruhusu matengenezo.
“Sababu ni kuruhusu matengenezo ya bomba kubwa la inchi 36 eneo la Visiga Saheni na kutoa matoleo mawili maeneo ya Kwembe na Msigani yanayolenga kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji maeneo ya Kibamba Pangaboy na Mbezi Malamba Mawili,” imeeleza taarifa.
Maeneo yaliyotajwa kuathirika ni pamoja na Chalinze, Chalinze Mboga, Msoga, Ruvu Darajani, Ruvu JKT, Vigwaza, Mlandizi, Mbwawa, Visiga, Maili 35, Misugusugu, Kongowe, Soga, Miembe Saba, Kwa Mfipa, Mwendapole, Tanita, Kwa Mathias na Kwa Mbonde.
Kampuni ya Australia iliyofutiwa leseni yatishia kuikamata ndege ya Tanzania
Maeneo mengine ni Picha ya Ndege, Lulanzi, Kibaha, Kiluvya, Kibamba, Mloganzila, Mbezi Magari Saba, Mbezi Kwa Yusufu, Njeteni, Msigani, Kifuru, Mbezi Inn, Mbezi Stendi ya Magufuli, Mbezi Mshikamano, Mbezi Louis, Makabe, Msakuzi, Mbezi, Kimara,Tabata, Segere, Kinyerezi, Kisukuru na Bonyokwa.
Pia wateja wa Kimara B, Kimara Korogwe, Bucha, Baruti, Ubungo, Magomeni, Ukonga, Uwanja wa Ndege, Kiwalani, Vingunguti, Gongo la Mboto, Pugu na Kisarawe watakumbwa na katizo hilo la maji.