Mafunzo urushaji drones kuanza Januari 4, wahitimu kutumia vyeti kuomba leseni

0
58

Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (Civil Aviation Training Centre) kilichopo jengo la zamani la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)- terminal one, kinatarajia kutoa mafunzo ya urishaji wa ndege zisizo na rubani yaani Drones Pilot Training) kuanzia Januari 4, 2021.

Taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) inaeleza kuwa mafunzo hayo yataendeshwa kwa kushirikiana na Chuo cha Prowings Training Limited cha Afrika Kusini, na yatakuwa kwa muda wa wiki nne, saa sita kwa siku (saa 2 asubuhi hadi saa 9 alasiri).

Sifa za mwombaji awe amemaliza kidato cha nne au zaidi, ajue kusoma na kuandika kiingereza na
pia awe na umri kuanzia miaka 21.

Mafunzo yataendeshwa kwa nadharia darasani na kwa vitendo katika viwanja vya Tanganyika Parkers – Kawe.

Kinadharia washiriki watajifunza kuhusu:
• Sheria za usafiri wa anga
• Uelewa wa ndege zisizokuwa na rubani
• Uwezo wa ndege, mipango na upangaji wa mizigo
• Hali mbalimbali za kiutendaji zinazoweza kuhatarisha shughuli za urushaji wa ndege zisizo na ruba
• Hali ya hewa
• Mifumo ya ndege zisizokuwa na rubani inayoiwezesha kupaa angani
• Taratibu na shughuli za urushaji wa ndege zisizokuwa na rubani
• Kanuni za urukaji wa ndege zisizokuwa na rubani
• Mawasiliano ya sauti kwa wana anga

Ada kwa mafunzo ni TZS 1,980,000/= ambayo itajumuisha chai ya saa nne, chakula cha mchana, vifaa vya kufundishia na gharama za usafiri kwenda viwanja vya Tanganyika peckers kwa ajili ya
mafunzo kwa vitendo.

Baada ya mafunzo wahitimu watatunukiwa vyeti vitakavyowawezesha kuomba leseni ya urushaji wa ndege hizo kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).

Send this to a friend