Magari 1500 yakamatwa kwa kufunga ving’ora

0
42

Jeshi la Polisi kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani limekamata jumla ya magari 1527 yanayohusisha magari madogo na malori yakiwa na vimulimuli na ving’ora kinyume na sheria na kanuni za usalama barabarani.

Akieleza Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Wilbrod Mutafungwa amesema kuwa magari yanayopaswa kuwa na ving’ora na vimulimuli vya dharura ni magari ya kubeba wagonjwa (Ambulance), magari ya Zimamoto na  magari ya vyombo vya ulinzi na usalama.

“Kama kuna mtu yeyote anahitaji kutumia ving’ora kwa dharura anatakiwa kuomba kibali kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi au kwa Jeshi la Polisi, iwapo atakubaliwa atasindikizwa kwa kutumia ving’ora na sio vinginevyo,” ameeleza Mutafungwa

Aidha kwenye taarifa yake amefafanua kuwa idadi ya pikipiki na bajaji zilizokamatwa zikiwa na vimulimuli na ving’ora visivyo rasmi ni 1358, huku idadi ya magari ya watu binafsi na ya serikali yaliyokamatwa yakitumia namba bandia ni 73

Send this to a friend