Magari ya masafa marefu kufungwa kamera kudhibiti uvunjifu wa sheria

0
57

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imesema imepanga kuweka kamera katika magari ya masafa marefu ili kudhibiti uvunjifu wa sheria unaofanywa na baadhi ya madereva pamoja na kuimarisha usalama wa abiria.

Mkurugenzi wa Udhibiti Usafiri wa Barabara, Johansen Kahatano amesema utaratibu huo unatarajiwa kuanza kabla ya Julai mwaka huu ambapo kwa sasa LATRA inaboresha kanuni za leseni ya usafirishaji magari ya abiria.

“Katika uboreshaji huo, tunataka magari ya masafa marefu yawe na kamera ndani yake ili kumwonesha dereva na abiria waliomo ndani na nje ya gari. Lengo hapo ni kutaka kugundua vitendo vya uvunjifu wa sheria lakini kuona namna dereva anavyoendesha gari lake,” amesema.

Bunge la Ghana lakatiwa umeme kwa kutolipa deni

Ameongeza kuwa “baada ya kufungwa kamera tutakuwa tunauwezo wa kufuatilia na kuona kila kitu kinachoendelea ni kama vile ilivyo ‘VTS’ (mfumo wa kufuatilia safari ya basi) japokuwa hali yenyewe itakuwa kwa kuona kwa macho kila kitu kinachoendelea kwenye gari.”

Aidha, amesema faida nyingine ya kamera hizo ni kufahamu gari zinazozidisha abiria, kurahisisha uchunguzi wa ajali, kufahamu kilichotokea barabarani, hali ya dereva hadi kutokea kwa ajali, kufahamu idadi ya abiria pamoja na kupunguza vihatarishi vya ajali hiyo.

Send this to a friend