Magari ya mizigo kutozwa ada ya usafi hadi TZS 50,000 kwa siku Ubungo

0
40

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo mkoani Dar es Salaam imetangaza viwango vya kibali cha usafi wa mazingira kwa magari yote yenye uzito kuanzia tani 0.5 yanayoingia kwenye manispaa hiyo kupaka au kushusha mizigo.

Viwango vya malipo hayo ni kulingana na ukubwa wa gari ambapo vinaanzia TZS 3,000 hadi TZS 50,000.

Aidha, taarifa ya manispaa imeeleza adhabu ya kutolipa ada hiyo ni kati ya TZS 300,000 hadi 1,000,000 au kifungo cha miezi sita au vyote kwa pamoja.

Send this to a friend