Magufuli: Msichague wagombea ambao hawatimizi ilani ya CCM

0
44

Mgombea wa Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Magufuli amewataka Watanzania kutomchagulia watu ambao hawatatimiza ilani ya chama hicho.

Akizungumza na mamia ya wananchi waliokusanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Somanda mkoani Simiyu, Dkt. Magufuli amesema anataka kumalizia miradi mbalimbali ya maendeleo, hivyo anataka watu watakaomsililiza, ambao ni wabunge na na madiwani.

“Msinichagulie watu ambao hawatatimiza ilani ya CCM, na sitakuwa na cha kuwafanya,” amesema mgombea huyo akiomba kura kwa wananchi hao.

Dkt. Mgombea huyo ameendelea na ziara ya kampeni mkoani Shinyanga na Simiyu ambapo atamalizia ziara yake kwa leo Butiama mkoani Mara.

Send this to a friend