Mahakama: Kesi ya kupinga uwekezaji bandarini haina mashiko

0
51

Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya imebariki mkataba uwekezaji bandarini na kusema ni halali na kwamba malalamiko yaliyowasilishwa mahakamani hapo na walalamikaji wanne ambao walidai mkataba huo unaenda kinyume na matakwa ya Katiba, hayana mashiko yoyote.

Akisoma hukumu hiyo, Jaji Dastan Ndunguru amesema baada ya jopo la majaji wa tatu kusikiliza pande zote mbili, mahakama imeamua kutupilia mbali malalamiko hayo yaliyowasilishwa mahakamani wakidai mkataba kukiuka sheria, kwenda kinyume na maslahi ya umma na rasilimali, mkataba kuhatarisha usalama na kuridhiwa bila ushiriki wa wananchi, amesema hoja hizo zote hazina mashiko.

Aidha, baada ya mahakama kutoa uamuzi huo, walalamikaji katika kesi hiyo wamesema wanajipanga kukata rufaa kupinga uamuzi huo.

“Tumesikia kigugumizi cha Mahakama, tumeshamwelekeza wakili wetu tutakata rufaa na tutawasilisha leo hii notisi ya kukata rufaa,” amesema Alphonce Lusako ambaye ni mlalamikaji wa kwanza katika kesi hiyo.

Benki ya Dunia yasitisha mikopo kwa Uganda kutokana na sheria ya kuzuia mapenzi ya jinsia moja

Naye Wakili aliyesimamia upande wa walalamikaji katika kesi hiyo, Boniphace Mwabukusi amesema wanatoa siku 14 Serikali kubadili mkataba huo.

“Kwa kuwa Mahakama imesema haina mamlaka ya kuingilia shughuli za Bunge sasa sisi tunakwenda kutumia Civil Bunge (Bunge la Wananchi) tutatoa siku 14 wabadili mkataba huu,”amesema.

Send this to a friend