Mahakama Kuu yawafutia hukumu Mbowe na wenzake, yaamuru faini zao kurejeshwa

0
70

Mahakama Kuu imetengua hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyowatia hatiani Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake saba, na kumriwa kulipa faini TZS milioni 350 au kwenda jela kwa miezi mitano kila mmoja.

Mbali na kutengua hukumu hiyo, Mahakama Kuu imemauru viongozi hao kurejeshewa faini TZS milioni 350 waliyolipishwa baada ya kutiwa hatiani.

Viongozi walitiwa hatiani Machi 10, 2020 kwa makosa 12 kati ya 13 ambayo walishtakiwa kwayo Februari 2018. Makosa hayo ni pamoja na kuitisha maandamano bila kibali na kusababisha vurugu.

Mbali na Mbowe, wengine walioshitakiwa katika kesi hiyo ni Dkt. Vicent Mashinji (sasa mwanachama wa CCM), Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Mwalimu, Salum Mwalimu (Zanzibar), Mchungaji Peter Msigwa na John Heche.

Wengine ni Wabunge Esther Matiko, Halima Mdee na Ester Bulaya.

Wakati kesi hiyo ikiendelea, wanasiasa hao waliituhumu serikali kuwa inatumia mahakama kama njia ya kuminya viongozi wa upinzani.

Send this to a friend